1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COTONOU: Akali watu 90 wamefariki, ndege moja ya abiria ilipopata ...

26 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFpI
ajali na kuanguka nchini Benin. Watu 18 wamenusurika, ndege BOEING 727 ilipoanguka, - alisema waziri wa afya wa Benin, Celine Segnon. Kwa mujibu wa wasimamizi wa safari za ndege mjini Cotonou, ndege hiyo ya shirika UTA ilikuwa ikielekea Beirut nchini Libanon, na pengine ilipata shida wakati wa kunyanyuka. Baada ya kuanza safari yake mjini Cotonou iligusa jengo moja, ikaripuka na ikaangukia baharini. Abiria wengi walikuwa Walibanon wakielekea nyumbani kutumia likizo zao.