1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COP28 kujikita kwenye uchafuzi wa vyombo vya usafiri

6 Desemba 2023

Mazungumzo katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) unaoendelea huko Dubai utajikita hii leo na masuala ya uchafuzi utakanao na vyombo vya usafiri pamoja na mazingira ya mijini.

https://p.dw.com/p/4ZpQg
Wanaharakati wakiandamana nje ya ukumbi wa mikutano ya COP28 kupinga kuendelea kutumiwa kwa nishati za visukuku.
Wanaharakati wakiandamana nje ya ukumbi wa mikutano ya COP28 kupinga kuendelea kutumiwa kwa nishati za visukuku.Picha: Amr Alfiky/REUTERS

Mjumbe wa hali ya hewa wa Marekani, John Kerry, anatarajiwa kuhutubia waandishi wa habari huku Rais wa COP28, Sultan Al-Jaber, akitarajiwa kuhutubia mkutano huo unaopangwa kumalizika Desemba 12.

Soma zaidi: Papa Francis awarai viongozi wa dunia kupambana na mabadiliko ya tabianchi

Wajumbe wanatarajia pia kuafikiana kuhusu rasimu ya awali itakayowasilishwa kwa mawaziri hasa kwa kuzingatia mambo kama kusitisha au kupunguza matumizi ya mafuta ya visukuku.

Rasimu hiyo itahitaji kutiwa saini na wajumbe wa mataifa karibu 200 wanaoshiriki mkutano huo.