CONAKRY.Maelfu ya watu washiriki kwenye maandamano
12 Februari 2007Matangazo
Takriban watu watatu wameuwawa kufuatia maandamano makubwa katika miji ya Conakry na mji wa mashariki wa Kankan nchini Guinea.
Maelfu ya watu wameandamana huku waporaji wakitumia vurugu hizo kuvunja maduka na kupora mali.
Mgomo ulioitishwa na viongozi wa vyama mbalimbali umeathiri sehemu nyingi za taifa hilo la Afrika Magharibi katika juhudi za kutaka kumng’oa mamlakani waziri mkuu Eugene Camara ambae ni chaguo la rais Lansana Conte.