1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOGNE: Waumini wakusanyika kwa Siku ya Vijana

16 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEkd

Zaidi ya waumini 400,000 kutoka sehemu mbali mbali za dunia wamemiminika katika mji wa Cologne nchini Ujerumani kuhudhuria Siku ya Vijana Duniani.Sherehe zitafunguliwa rasmi leo jumanne,kwa misa zitakazosomwa kwenye viwanja vya mpira vya Cologne,Düsseldorf na katika Uwanja wa Bustani mjini Bonn.Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 anatarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa Cologne-Bonn siku ya Alkhamis chini ya ulinzi mkali.Hii itakuwa ziara yake ya kwanza ya kigeni tangu kushika hatamu za kuliongoza Kanisa Katoliki.Siku ya jumapili,Baba Mtakatifu atasoma misa katika uwanja mkubwa wa Marienfeld,nje ya Cologne.Inakadiriwa kuwa misa ya siku ya jumapili,itahudhuriwa na zaidi ya waumini 800,000.