1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yatoa mwito kwa jumuiya ya BRICS kutimiza dhima kubwa

11 Juni 2024

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi ametoa wito huo wakati ambapo nchi za magharibi zimeweka vikwazo na vizingiti vya biashara dhidi ya nchi yake.

https://p.dw.com/p/4gvHh
Waziri wa Mambo ya nje wa China Wang Yi
Waziri wa Mambo ya nje wa China Wang YiPicha: Murat Gok/Anadolu/picture alliance

Kampuni kadhaa za China zinakabiliwa na vikwazo vya nchi za magharibi kutokana na msimamo wa China wa kuiunga mkono Urusi katika vita vyake vya nchini Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa China alikuwapo mjini Nizhny Novgorod, nchini Urusi kuhudhuria mkutano na mwaziri wanzake wa mambo ya nje wa Urusi, Brazil, India na Afrika Kusini.

Waziri Wang amesema jumuiya ya BRICS, iliyopanuka inapaswa kujenga mkakati wa ushirikiano katika msingi wa masoko ya nchi zinazoinukia duniani.