1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rais wa China afanya mazungumzo na waziri mkuu wa Pakistan

7 Juni 2024

Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo na waziri mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharrif mjini Beijing leo.

https://p.dw.com/p/4gnmp
Rais wa China Xi Jinping awakiwa na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif
Rais wa China Xi Jinping awakiwa na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz SharifPicha: China Daily/REUTERS

Mzungumzo haya yanafanyika ikiwa ni siku kadhaa kabla ya Pakistan kutangaza bajeti yake ya kila mwaka na hatua ya kupeleka ombi jipya la kuomba mkopo katika shirika la fedha la kimataifa IMF.

Serikali ya waziri mkuu Sharif inatarajia kuomba takriban dola bilioni 6 chini ya mpango mpya wa IMF baada ya kuwasilisha bajeti yake ya mwaka ambayo kwa mujibu wa vyanzo huenda ikatangazwa Juni 10.

Soma pia:Kundi la Taliban lauteka mji wa 10 Afghanistan

Mkopo wa dola bilioni 27 ambazo Pakistan inadaiwa na China ndiyo suala kuu litakaibuka katika mazungumzo ya viongozi wa Islamabad na IMF.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW