1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

China yaikosoa Marekani kwa kuyashtaki makampuni yake

24 Juni 2023

China imezikosoa mamlaka za Marekani kwa kuzishtaki kampuni nane na raia wanne wa China kwa tuhuma za kufanya ulanguzi wa kemikali zinazotumika kutengeneza dawa ya kupunguza maumivu ya Fentanyl.

https://p.dw.com/p/4T1Cv
Fentanyl Droge
Picha: Craig Kohlruss/ZUMA Wire/IMAGO

China imesema ilichokifanya Marekani ni ukamataji holela. Wizara ya haki ya Marekani imekuwa ikifanya juhudi za kuitokomeza dawa hiyo ambayo matumizi yake mabaya yanadaiwa kusababisha vifo nchini humo kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.

Dawa hiyo inatajwa kuwa na nguvu mara 50 zaidi ya dawa za kulevya aina ya heroin. Hatua hiyo ni ya kwanza ya hivi karibuni kwa Marekani kuyashitaki makampuni ya China kwa kufanya ulanguzi wa kemikali za kutengeneza Fentanyl nchini humo. Mexico ndiyo inayofahamika zaidi kwa kuziingiza Marekani kwa njia ya ulanguzi kemikali hizo.