1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China kushiriki mazungumzo kuhusu mpango wa amani wa Ukraine

5 Agosti 2023

China itamtuma afisa wa ngazi ya juu kushiriki mazungumzo ya kusaka amani ya Ukraine yanayofanyika mwishoni mwa juma hili nchini Saudi Arabia.

https://p.dw.com/p/4Uo0V
Die Fahnen von China und der Ukraine nebeneinander
Picha: Viacheslav Chernobrovin/Zoonar/picture alliance

Mazungumzo hayo yaliyoitishwa na Saudia, yanatarajiwa kufanyika mjini Jeddah kuanzia leo na kuwakutanisha wanadiploamsia wa Ukraine, nchi za Magharibi, washauri wa kitaifa wa usalama na maafisa waandamizi kutoka nchi takribani 40.

Soma zaidi: China yatoa wito wa kuanzishwa tena usafirishaji wa nafaka

Wajumbe katika mazungumzo hayo ya siku mbili watakubaliana juu ya mpango wa amani wa kumaliza vita ya Urusi nchini Ukraine. Rais Volodmyr Zelensky amesema mapema wiki hii kwamba ana matumaini mpango huo utafungua njia kuelekea mkutano wa kilele wa amani wa viongozi wa ulimwengu baadae mwaka huu ili kujadili vipengele vya utatuzi wa mzozo na Jirani yake.

Urusi haikualikwa katika mazungumzo ya mjini Jeddah. Saudi Arabia imejitolea mara kwa mara kupatanisha Urusi na Ukraine.