1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Wito kutolewa kwa China kuisaidia Ukraine

21 Juni 2023

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamejiandaa kuitolea mwito China wiki ijayo kusaidia kumaliza vita nchini Ukraine na kuweka urari wa kiuchumi katika mahusiano yake na Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4SskA
EU-Haushalt
Picha: Virginia Mayo/dpa/picture alliance

BRUSSELS,

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamejiandaa kuitolea mwito China wiki ijayo kusaidia kumaliza vita nchini Ukraine,kujihusisha katika changamoto za ulimwengu,kama vile mazingira na kuweka  urari wa kiuchumi katika mahusiano yake na Umoja wa Ulaya.

Agenda kuu ya mkutano ni China na usalama wa kiuchumi

Hayo yameelezwa na afisa mmoja mwandamizi katika Umoja huo wa Ulaya.Viongozi watakutana Brussels katika mkutano wa kilele Juni 29 mpaka 30,huku China na suala la usalama wa kiuchumi zikiwa ajenda kuu.

Nchi za Magharibi zinaitaka China kutumia ushawishi wake kuelekea Urusi 

Afisa Mwandamizi wa Umoja wa Ulaya amesema viongozi watakaokutana huenda kwenye mazungumzo yao, wakajikita zaidi kwenye suala la dhima ya China kuelekea uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na mahusiano ya kiuchumi. Nchi za Magharibi zinaitaka China kutumia ushawishi wake kuelekea Urusi kusimamisha vita.