1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Chama tawala cha Afrika Kusini chaelekea kupoteza wingi

31 Mei 2024

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) kimepata chini ya asilimia 42 ya kura baada ya zaidi ya asilimia 55.63 ya kura kuhesabiwa mpaka sasa.

https://p.dw.com/p/4gUEE
Uchaguzi nchini Afrika Kusini 2024
Mmoja ya wapiga kura nchini Afrika Kusini akiwa amevaa kanga yenye picha ya mgombea kupitia chama cha ANC Cyril RamaphosaPicha: Siphiwe Sibeko/REUTERS

Kwa mara ya kwanza tangu chama cha ANC kiingie madarakani miaka 30 iliyopita, huenda kikapungukiwa na viti vya kukiwezesha kulidhibiti bunge na hivyo kulazimika kuingia katika serikali ya mseto.

Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance mpaka sasa kimefikia asilimia 23.7 huku chama cha uMkhoto weSizwe cha rais wa zamani, Jacob Zuma kikiwa na asilimia 10.8, na kile cha wapigania ukombozi wa kiuchumi, EFF cha Julius Malema kikifikia asilimia 9.6 ya kura.

Matokeo kamili yanatarajiwa kufahamika mwishoni mwa wiki.