1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANC yaelekea kupoteza wingi wa kura Afrika Kusini

30 Mei 2024

Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu uliofanyika jana nchini Afrika Kusini yanaonesha chama tawala cha African National Congress kimeambulia chini ya asilimia 50 ya kura.

https://p.dw.com/p/4gT1C
Wapiga kura wakiwa katika zoezi la kuchagua wabunge.
Wapiga kura wakiwa katika zoezi la kuchagua wabunge.Picha: Zinyange Auntony/AFP

Matokeo hayo yanayoongeza uwezekano kwa chama hicho kupoteza kwa mara ya kwanza wingi wa viti bungeni tangu kiliposhika hatamu za dola miaka 30 iliyopita. 

Hadi sasa katika asilimia 20 ya kura zilizokwishahesabiwa, ANC kimepata asilimia 43 kikifuatiwa na chama cha Democratic Alliance kinachokaribia asilimia 30. 

Soma pia:Afrika Kusini yasubiri matokeo ya uchaguzi mkuu

Chama cha mwanasiasa machachari Julius Malema na kile cha rais wa zamani Jacob Zuma cha uMkhonto weSizwe vimeambulia chini ya asimilia 10 ya kura. 

Iwapo ANC itashindwa kupata asilimia 50 ya kura italazimika kutafuta mshirika kutoka vyama vingine vidogo ili kuunda serikali. Matokeo hayo yatadhihirisha kuanguka kwa umashuhuri wa chama hicho tangu kulipoingia madarakani mwaka 1994 chini ya hayati Nelson Mandela.