1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Labour chazindua ilani kuelekea uchaguzi Uingereza

14 Juni 2024

Chama kikuu cha upinzani nchini Uingereza cha Labour kimezindua ilani yake ya uchaguzi kikiahidi kuufufua uchumi wa nchi hiyo iwapo kitashinda uchaguzi wa mwezi unaokuja.

https://p.dw.com/p/4h15S
Kiongozi wa chama cha Labour Keir Starmer
Kiongozi wa chama cha Labour Keir Starmer.Picha: Gareth Fuller/AP Photo/picture alliance

Ilani hiyo iliyopachikwa jina la "ahadi ya kutengeneza utajiri" imezinduliwa wakati chama hicho kinaongoza kwa wingi wa asilimia katika uchunguzi wa maoni ya umma. Takwimu hizo zinatoa matumaini kwamba huenda kitapata ushindi na kuhitimisha miaka 14 ya kuwa upande wa upinzani.

Kiongozi wa Labour Keir Starmer ambaye atakuwa Waziri Mkuu iwapo chama chake kitashinda amesema kuwatajirisha Waingereza na kuufufua uchumi ndiyo itakuwa ajenda ya kipaumbele.

Uchaguzi mkuu wa Uingereza utafanyika Julai 4 ambapo chama tawala cha Conservative kinatetea nafasi yake chini ya Waziri Mkuu Rishi Sunak.