1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rishi Sunak aitisha uchaguzi mkuu Uingereza

23 Mei 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ameitisha uchaguzi mkuu Julai 4, akisema Waingereza wataweza kuchagua mustakbali wao katika kura ambayo chama chake kinatazamiwa kupoteza madaraka.

https://p.dw.com/p/4gAUj
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi SunakPicha: Hollie Adams/REUTERS

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ameitisha uchaguzi mkuu Julai 4, akisema Waingereza wataweza kuchagua mustakbali wao katika kura ambayo chama chake cha Conservative kinatazamiwa pakubwa kushindwa na chama cha upinzani cha Labour, baada ya kukaa madarakani kwa miaka 14.

Kulingana na uchunguzi wa maoni ya wapigakura, chama cha Labour kinaongoza mbele ya Conservative kwa takribani asilimia 20. Kiongozi wa Labour Keir Starmer, amesema uchaguzi huo unamaanisha "fursa ya mabadiliko."

Chama cha Conservative kimekuwa madarakani tangu 2010 na Sunak ndiye waziri mkuu wa tatu wa Conservative tangu uchaguzi wa mwisho wa mwaka 2019, kilipopata wingi wa viti 80 bungeni.