1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Chama cha ANC chahitaji washirika kuunda serikali ya mseto

Saleh Mwanamilongo
2 Juni 2024

Chama tawala cha Afrika Kusini cha African National Congress ANC kimepoteza wingi wa viti bungeni kwa mara ya kwanza mnamo kipindi cha miongo mitatu.

https://p.dw.com/p/4gXpA
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma Picha: Emilio Morenatti/AP Photo/picture alliance

Chama hicho kimehitaji washirika ili kuunda serikali ya mseto. Matokeo ya awali ya tume ya uchaguzi yameonyesha chama cha ANC kikipata asilimia 40.2 ya kura. Huku chama kikuu cha upinzani cha Democtratic Alliance DA kikiwa na asilimia 21.

Wakati chama kilichoanzishwa miezi sita iliyopita na rais wa zamani Jacob Zuma, uMkhonto we Sizwe (MK), kikishika nafasi ya tatu na asimilia 14.5.

Na Chama chenye ushawishi wa Marxist cha Wanaopigania Uhuru wa Kiuchumi (EFF) kimepata asilimia 9.5 ya kura. Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yatatolewa baadaye leo.