ANC yaonekana kushindwa kupata wingi wa viti bungeni
1 Juni 2024ANC imekuwa ikishinda katika kila chaguzi ya kitaifa nchini humo tangu uchaguzi wa kihistoria uliofanyika mwaka 1994 uliomaliza utawala wa wazungu.
Lakini ndani ya muongo mmoja uliopita umaarufu wake ulianza kushuka baada ya waafrika kusini kushuhudia uchumi kuyumba na kutokuwa inavyohitajika, kupanda kwa viwango vya ukosefu wa ajira, na uchakavu wa miundo mbinu.
Huenda Afrika Kusini ikaunda serikali ya mseto
Matokeo yanayoendelea kutolewa baada ya kura kuhesabisha katika zaidi ya asilimia 97 kati ya vituo 23,000 vya kupigia kura katika uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumatano, ANC imepata asilimia 40.11 ya kura ikiwa imeshuka kutoka asilimia 57.50 iliyopata katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2019.
Chama kikuu cha upinzani cha the Democratic Alliance, kimepata asilimia 21.72 ya kura zilizohesabiwa hadi sasa huku chama cha uMkhonto we Sizwe (MK), chama kipya kinachoongozwa na rais wa zamani Jacob Zuma kikipata asilimia 14.83 ya kura.