1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha ANC kiko tayari kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa

7 Juni 2024

Chama tawala nchini Afrika Kusini, African National Congress ANC kimetangaza kwamba kitaunda serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya kupoteza nafasi ya kuwa chama chenye wingi mkubwa bungeni.

https://p.dw.com/p/4gmQv
Johannesburg, Afrika Kusini | Rais Cyril Ramaphosa,
Rais wa Afrika Kusini Cyril RamaphosaPicha: Zhang Yudong/Xinhua/picture alliance

Rais wa nchi hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha ANC Cyril Ramaphosa amewaambia waandishi habari baada ya kuwa na mkutano na uongozi wa chama hicho jana jioni,kwamba wamekubaliana kuvialika vyama vyote katika mchakato wa kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa. 

Ramaphosa amesema hatua hiyo ndiyo bora zaidi ya kuifanya nchi hiyo kusonga mbele.

Pendekezo hilo la ANC linamaanisha Afrika Kusini inataka kuwa na serikali ya mseto itakayojumuisha vyama vyote vilivyopata viti katika bunge la nchi hiyo wakati wa uchaguzi. 

Soma pia: Chama cha ANC chasaka kuunda serikali ya umoja wa kitaifa


Chama hicho kimesema serikali ya Umoja wa Kitaifa itawakilisha maslahi ya wapiga kura wote.

Wachambuzi lakini wana wasiwasi kwamba  serikali ya Umoja wa Kitaifa huenda ikashindwa  kupata uthabiti wa taifa na kushindwa kufikia makubaliano.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW