1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroChad

Chad kuwasindikiza wanajeshi wa Ufaransa kutoka Niger

13 Oktoba 2023

Kutoka N'Djamena wanajeshi wa Ufaransa wanaweza kuondoka kwa njia ya ndege na vifaa vyao vya kisasa.

https://p.dw.com/p/4XVox
Wanajeshi wa Ufaransa waanza kuondoka Niger kwa kupitia Chad
Wanajeshi wa Ufaransa waanza kuondoka Niger kwa kupitia ChadPicha: Dominique Faget/AFP

Chad inasema jeshi lake litawasindikiza wanajeshi wa Ufaransa walioamriwa waondoke kutoka nchi jirani ya Niger na utawala wa kijeshi watakapopitia nchi hiyo wakiwa njiani kurejea kwao.

Jeshi la Ufaransa linakabiliwa na kazi ya kusafirisha vifaa vyake kwa njia ya ardhi kupitia Chad na baadaye Cameroon - umbali wa zaidi ya kilometa 3,000, ambazo sehemu zinafahamika kuwa maficho ya makundi ya wapiganaji wa jihad.

Kikosi cha kwanza kilianza safari kutoka kambi yao huko Ouallam kuelekea nchi jirani ya Chad siku ya Jumanne, wakisafiri kwa njia ya barabara na magari yasiyoweza kutobolewa na risasi wakisindikizwa na wanajeshi wa Niger.

Kutoka N'Djamena wanajeshi wa Ufaransa wanaweza kuondoka kwa njia ya ndege na vifaa vyao vya kisasa.