1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Niger yamfukuza mratibu wa Umoja wa Mataifa

12 Oktoba 2023

Viongozi wa kijeshi wa Niger wamemuamuru mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini humo kuondoka ndani ya masaa 72.

https://p.dw.com/p/4XRBr
Louise Aubin, mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Niger
Louise Aubin, mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini NigerPicha: UN

Viongozi hao wameulaumu umoja huo kwa kuzuwia kutambuliwa kwa serikali yao iliyoingia madarakani baada ya mapinduzi.

Amri hiyo imetangazwa siku moja tu baada ya Marekani kuzuwia msaada wa zaidi ya dola milioni 500 kwa Niger, huku Ufaransa ikianza kuondosha wanajeshi wake baada ya nao kuamuriwa kuondoka na watawala wapya wa Niamey.

Kwenye taarifa yake, wizara ya mambo ya nje ya Niger imesema serikali inamfukuza Louise Aubin, mratibu mkaazi wa Umoja wa Mataifa, na kumuagiza kuchukuwa hatua zote muhimu zinazomuwezesha kuondoka kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi ndani ya siku tatu kuanzia Jumanne ilipoandikwa taarifa hiyo.

Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa imethibitisha kutolewa kwa amri hiyo.