CENI yatangaza matokeo ya uchaguzi wa bunge wa DRC
29 Desemba 2011Matangazo
Mwanzoni CENI ilikuwa imesitisha shughuli za kuhesabu kura za uchaguzi wa Bunge, uliofanyika tarehe 28 Novemba sambamba na ule wa urais, ikisubiri ujio wa wataalamu wa kimataifa kuisaidia kutatua yale iliyoyaita kuwa ni 'matatizo ya kiufundi'. Lakini sasa Tume hiyo imeanza tena shughuli hiyo licha ya kutokuwasili kwa wataalamu hao.
Matokeo ya zaidi ya majimbo 60 miongoni mwa majimbo 169 ya kura yanaonyesha kuweko kwa ushindani baina ya vyama vikuu viwili, huku vigogo wengi wa chama tawala wakishindwa kupata ushindi kwenye uchaguzi huo, kama anavyoripoti Saleh Mwanamilongo kutoka Kinshasa.
Mwandishi: Saleh Mwanamilongo
Mhariri: Saumu Yusuf