1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CANBERRA: Serikali ya Australia imekubali kimsingi kushiriki katika mfumo

4 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFvH

unaokuzwa na Marekani wa kujilinda hewani dhidi ya hujuma za maroketi. Waziri wa kigeni Alexander Downer alitangaza bungeni mjini Canberra, Australia inalazimika kujilinda dhidi ya kitisho hiki. Kwa mujibu wa magazeti ya kijapani, serikali mjini Tokio kadhalika imeazimia kujiunga na mfumo wa kujikinga na maroketi ya Korea Kaskazini. Baraza la mwaziri litapitisha uamuzi karibuni.