1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niger, Burkina Faso na Mali zaunda jeshi la pamoja

25 Agosti 2023

Jeshi la Niger limeunda muungano wa kijeshi na nchi jirani za Burkina Faso na Mali ambazo watawala wake pia walichukua madaraka kwa njia ya mapinduzi

https://p.dw.com/p/4VZce
Pro-Putsch-Demo in Nigers Hauptstadt Niamey
Raia wa Niger wakiwa kwenye maandamano ya kulipinga jeshi la Ufaransa kuingilia kati mapinduzi ya kijeshi nchini humo. Picha: AFP/Getty Images

       

Jeshi nchini Niger ambalo lilichukua mamlaka nchini humo katika mapinduzi ya Julai 26, limeunda muungano wa kijeshi na nchi jirani za Burkina Faso na Mali ambazo watawala wake pia walichukua madaraka kwa njia ya mapinduzi. Viongozi wa kijeshi wa Niger wameidhinisha kuwa vikosi vya Mali na Burkina Faso vitaisaidia endapo nchi hiyo itashambuliwa.

Soma zaidi :Niger yaidhinisha wanajeshi wa Mali na Burkina Faso

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na nchi hizo tatu Niger, Burkina Faso naMaliinaashiria kwamba viongozi wa mapinduzi wa Niger wanapanga kuendelea kukataa shinikizo la kikanda la kuachia madaraka.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo tatu walikutana mjini Niamey jana ili kujadili ushirikiano zaidi wa kiusalama pamoja na masuala mengine. Burkina Faso na Mali zimesisitiza msimamo wao wa kukataa uingiliaji wowote wa kijeshi dhidi ya Niger ukiutaja kama tangazo la vita dhidi yao.

ECOWAS: Kuna haja ya kulinda mipaka yetu dhidi ya ugaidi.

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika MagharibiECOWAS, imekuwa ikijaribu kufanya majadiliano na viongozi wa mapinduzi lakini imeonya kwamba iko tayari kupeleka wanajeshi nchini humo kwa lengo la kurejesha utulivu ikiwa juhudi za diplomasia zitashindikana.

Mazungumzo kati ya ECOWAS na utawala wa kijeshi wa Niger yalifanyika mwisho mwa wiki iliyopita. Makubaliano hayo yaliyotangazwa Alhamisi pia yanawataka watatu hao kuchukua hatua za pamoja dhidi ya makundi ya kigaidi yanayoendesha oparasheni zao huko na pia kulinda mipaka yao.

Kwa miaka mingi, nchi za ukanda wa Sahel zimekuwa zikitishiwa na
wanamgambo mbalimbali wa kigaidi, huku baadhi yao wakifungamanishwa na makundi ya Al-Qaeda na Dola ya Kiislamu.

Macron, ECOWAS ina mwendo wa kinyonga

Wakati hayo yakijiri, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron jana Alhamisi ametoa wito wa kurejea kwa utaratibu wa kidemokrasia na kuachiliwa kwa Rais Mohamed Bazoum, Mahusiano kati ya Ufaransa na Niger yamedorora tangu yalipofanyika mapinduzi ya kijeshi nchini Niger.

Paris Macron und Ehefrau Brigitte begrüßen Mohamed Bazoum Präsident von Niger
Rais Macron wa Ufaransa akiwa na mke wake pamoja na rais Mohamed Bazoum aliyepinduliwa na jeshi nchini Niger.Picha: Michel Euler/AP/picture alliance

Pamoja na uwepo wa jeshi la Ufaransa katika ukanda huo, rais Macron ameeleza kwamba bado ukanda wa nchi za Afrika magharibi hazijaonyesha nia ya kushirikiana ipasavyo na hivyo kubaki nyuma.

Soma zaidi: Ufaransa: Upo uwezekano wa suluhu ya mzozo wa Niger

Kwa upande mwingine, mataifa jirani kama algeria yamejitokeza kupinga tishio la jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS kutuma kikosi cha kijeshi kuingilia kati iwapo utawala mpya wa kijeshi utashindwa kurejesha utawala wa demokrasia na kwamba bado ipo nafasi ya mazungumzo ya kidiplomasia.

Mapinduzi ya kijeshi nchini Niger yalipata ungwaji mkono mkubwa wa raia nchini humo na wakati nchi za Burkina Faso na Mali zikionesha kuunga mkono kinachoendelea, raia nchini humo pia waanamini kundi la mamluki la Wagner licha ya kudaiwa kufariki kwa kiongozi wake Yevgeny Prighozhin bado waanamini kundi hilo litawasaidia kukabiliana na ushawishi wa mataifa ya magharibi.

 Baraou Souleimane raia wa Niger ambaye ni  mshonaji nguo anasema 

"Tunaomba kwamba Mwenyezi Mungu aimarishe uhusiano na (Wagner) ili kuendeleza mpango huo. Ikiwa uhusiano huo ni mzuri na wenye nguvu inawezekana wataendelea na mpango huo hata baada ya kifo chake (Yevgeny Prigozhin)``.

Nigeryenye idadi ya  wakaazi karibu milioni 26 ni moja ya nchi maskini zaidi duniani na chini ya utawala wa Mohammed Bazoum, Niger ilikuwa inatazamwa kuwa moja ya washirika wa mwisho wa kimkakati wa nchi za Magharibi katika mapambano dhidi ya ugaidi katika ukanda wa Sahel.