1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Biden akubali kukutana na Netanyahu nchini Marekani

18 Julai 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amekubali kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu baadae mwaka huu nchini Marekani.

https://p.dw.com/p/4U2Zq
Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa kongamano la viongozi wa Marekani na mataifa ya Nordic Helsinki
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Antti Aimo-Koivisto/Lehtikuva/dpa/picture alliance

Ombi hilo la mkutano baina ya viongozi hao wawili linakuja katika mkesha wa mkutano kati ya Biden na Rais wa Israel Isaac Herzog.

Mkutano kutuliza mvutano kwa kiasi fulani

Mkutano huo wa Biden na Netanyahu utatuliza kwa kiasi fulani mvutano baina ya viongozi hao wawili baada ya hivi majuzi, kusema kwamba Netanyahu anaongoza serikali ya muungano "yenye itikadi kali zaidi" kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha nusu karne.

Huu utakuwa mkutano wa kwanza kati ya Netanyahu na Biden  tangu waziri mkuu huyo aliporudi mamlakani.