1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga: Manuel Neuer arudi mazoezini

29 Agosti 2023

Mlinda lango wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani na klabu ya Bayern Munich Manuel Neuer amerudi katika mazoezi baada ya kuwa nje kutokana na jeraha la mguu.

https://p.dw.com/p/4VhJV
Manuel Neuer mit Torwart-Trainer Michael Rechner
Picha: Ulrich Wagner/picture alliance

Neuer alivunjika mguu mnamo Disemba wakati akicheza mchezo wa kuteleza juu ya theluji. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 37 amekuwa akifanya mazoezi ya binafsi ili kujiimarisha kimchezo baada ya Ujerumani kuondolewa katika kinyanganyiro cha Kombe la Dunia nchini Qatar.

Soma pia: Nahodha wa Bayern Munich Manuel Neuer afanyiwa upasuaji

Mtendaji mkuu wa Bayern Jan-Christian Dreesen amesema Neuer "ameimarika katika kupona jeraha" lakini hakuna tarehe maalum iliyowekwa ya kurudi kwake katika kikosi cha Bayern Munich.

Wakati huo huo kipa mpya wa akiba Daniel Peretz amesema hatokubali kukaa kando kama mchezaji wa akiba. Peretz mwenye umri wa miaka 23 amesajiliwa kwa kiasi kidogo cha fedha kutoka Maccabi Tel Aviv kama msaidizi wa Sven Ulreich wakati Neuer akiendelea kupata nafuu.

Peretz atafanyishwa mazoezi ili kuwa kipa wa pili baada ya Neuer, wakati Ulriech anafikia mwisho wa muda wake wa kucheza kandanda lakini kijana huyo kutoka Israel ana maono makubwa.

"Ninafurahia changamoto hii. Bila shaka nataka kucheza, nataka kuonyesha uwezo wangu," alisema wakati wa utambulisho kwake.

"Nimekuwa shabiki wa Bayern tangu nikiwa mtoto. Manuel ni mtu ninaye mtazama sana. Nilikutana naye jana. Yeye ni mkarimu sana na mtu mzuri."

Bayern ilimruhusu mrithi wa kwanza wa Neuer, Yann Sommer, kuondoka kwenda Inter Milan huku Alexander Nübel akitolewa kwa mkopo kuelekea Stuttgart.

"Daniel ana uwezo mkubwa. Nina hakika tunaweza kujipanga na Danieli kwa kutazama siku zijazo." Dreesen alisema.

Hatma ya Pavard

Pia alizungumzia mustakabali wa beki wa kulia wa Bayern wa timu ya taifa ya Ufaransa Benjamin Pavard, ambaye anataka kuondoka na anahusishwa na klabu ya Intermilan, akisema  "tuna siku chache. Tuna uhakika kwamba tunaweza kutatua suala hili wakati wa dirisha hili la uhamisho,"  na tarehe ya mwisho ya uhamisho ni  Ijumaa.

Deutschland Bundesliga Bayern München vs. RB Leipzig
Picha: Christian Kolbert/IMAGO

Iwapo Bayern watamuuza Pavard, wamehusishwa na usajili wa mchezaji wa Chelsea Trevor Chalobah na Lukas Kolostermann wa Leipzig wakati wakitafuta beki wa kulia na kujaza pia kama kiungo wa kati.

Konrad Laimer aliingia kama beki wa kulia kama mbadala wa Noussair Mazraoui wakati wa mechi dhidi ya Augsburg licha ya kusajiliwa kama kiungo wa kati. Kocha Thomas Tuchel ameashiria kwamba anahitaji kiungo mwengine wa kati.