1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS. Umoja wa Ulaya wataka mauzo ya nguo za China yadhibitiwe.

18 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFCV

Kamisheni ya Ulaya imeimarisha juhudi zake za kuidhibiti China dhidi ya uvamizi wa soko la nguo.

Brussels inataka kufanyike mzungumzo ya haraka ili kudhibiti kuingizwa kwa wingi katika soko la Umoja wa Ulaya nguo kutoka China.

Hatua hii inafuatia baada ya Washington kuamua kurudisha sheria za kikomo katika mauzo kwa bidhaa za aina tatu za nguo kutoka China hatua ambayo imepingwa vikali na serikali ya Beijing huku ikishutumu kuwa hatua hiyo inakiuka sheria za shirika la biashara duniani WTO na huenda ikavuruga maelewano ya kibiashara.

Wakati huo huo Makamu wa waziri mkuu wa China Wu Yi amewasili Japan kuanza ziara ya siku nane yenye azma ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.

Wu atakutana na waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi na maafisa wa kibiashara katika mazungumzo yatakayo lenga utatuzi wa mipaka ya bahari mashariki mwa China.

Lakini wadadisi wa mambo ya kisiasa wanasema kuwa hatua ya Beijing ya kumtuma makamu wa waziri mkuu wake nchini Japan badala ya waziri mkuu Wen Jiabao ambae ndio haswa alie alikwa na Japan inaonesha kama dharau.