1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS. Shughuli ya kupiga kura ya maoni kuendelea katika nchi za Umoja wa Ulaya.

31 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF8L

Rais wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Baroso amesema kuwa hakuna majadiliano mapya yatakayo anzishwa juu ya katiba ya Umoja huo hata baada ya Ufaransa kupiga kura ya hapana dhidi ya katiba hiyo.

Bwana Baroso amesema serikali za nchi wanachama 24 kati ya nchi 25 wanachama bado hazija toa ishara ya kuwa zinataka majadiliano hayo kuanza.

Taarifa yake imefuatia matokeo ya kura ya maoni juu ya katiba ya Umoja wa Ulaya iliofanyika huko Ufaransa jumapili iliyopita ambako asilimia 55 ilipinga azimio la kuanzishwa kwa katiba hiyo, hali ambayo imeutia dosari mchakato wa mataifa 25 ya umoja wa Ulaya.

Lakini kamishna wa maswala ya kibiashara wa Umoja wa Ulaya Peter Mandelson amesema shughuli hiyo ya kupiga kura ya maoni itaendelea.

Nchi tisa wanachama ikiwemo Ujerumani zimeunga mkono mswada wa katiba ya ulaya lakini katiba yenyewe ingefanya kazi tu kama ingekubalika na nchi zote 25 wanachama.