1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Nchi 16 zatishiwa kuchukuliwa hatua ya kisheria kwa kutotekeleza sheria za uhamiaji za Umoja wa Ulaya

3 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEVC
Koffi Annan
Koffi AnnanPicha: AP

Tume ya Umoja wa Ulaya imezitishia serikali za nchi 16 kwa hatua ya kisheria kwa kushindwa kutekeleza sheria za Umoja wa Ulaya zenye kuwaruhusu wahamiaji kuzileta familia zao kwenye nchi hizo.

Katika taarifa chombo hicho kikuu cha utendaji cha Umoja wa Ulaya kimesema nchi 16 kati ya 25 wanachama wa Umoja wa Ulaya zimeshindwa kuridhia sheria hizo kabla ya tarehe ya mwisho kutakiwa kufanya hivyo leo hii.Muongozo huo ulikubaliwa hapo mwaka 2003 kwa kuanzisha kanuni za pamoja kwa wahamiaji na wakimbizi wanaoloweya katika mataifa ya Umoja wa Ulaya kuwaingiza katika nchi hizo wake na watoto wao.

Uingereza,Denmark na Ireland hazikuhusishwa na muongozo huo wakati huo lakini miongoni mwa mataifa mengine 22 ya Umoja wa Ulaya ni Ubelgiji tu,Estonia,Latvia,Lithuania,Poland na Slovenia zimetekeleza sheria hiyo.