1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani ya Kusini

Bolsonaro achunguzwa kwa ufisadi wa dola 70,000

12 Agosti 2023

Polisi nchini Brazil inamtuhumu rais wa zamani wa nchi hiyo, Jair Bolsonaro, kupokea dola 70,000 za Kimarekani kwa mauzo ya saa mbili za kifakhari alizozawadiwa na Saudi Arabia wakati akiwa madarakani.

https://p.dw.com/p/4V5Yz
Rais wa zamani wa Brazil, Jair Bolsonaro
Rais wa zamani wa Brazil, Jair BolsonaroPicha: Chandan Khanna/AFP/Getty Images

Mapema hivi leo, maafisa wa polisi walivamia nyumba na ofisi za watu kadhaa wanaotuhumiwa kuhusika na mkasa huo, akiwemo jenerali mmoja wa juu jeshini. Mwenyewe Bolsonaro amekana kufanya kosa lolote kuhusiana na zawadi hizo. Afisa mmoja wa polisi ameliambia shirika la habari la AP kwamba wameomba ruhusa ya mahakama kuchunguza akaunti binafsi za benki na taarifa za fedha za Bolsonaro, na pia msaada wa shirika la ujasusi la Marekani, FBI.

Soma zaidi: Polisi wachunguza vito vya thamani vya Bolsonaro vilivyoingizwa Brazil

Kesi hii ni sehemu tu ya kesi nyengine kadhaa, ambazo rais huyo wa zamani wa Brazil anachunguzwa. Tayari anakabiliwa na uchunguzi juu ya ushiriki wake kwenye uvamizi uliofanywa na wafuasi wake dhidi ya mji mkuu na taasisi za serikali kupinga kushindwa kwake kwenye uchaguzi na kutangazwa kwa hasimu wake, rais wa sasa, Lula da Silva.