1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiTanzania

Benki Kuu ya Tanzania yasisitiza matumizi ya dijitali

31 Mei 2024

Benki Kuu ya Tanzania, BoT, imesisitiza matumizi ya dijitali katika utoaji wa huduma za kifedha kwa lengo la kuepusha mianya ya rushwa.

https://p.dw.com/p/4gVRS
Majengo pacha ya Benki Kuu ya Tanzania
Benki Kuu nchini Tanzania imehimiza matumizi ya dijitali katika utoaji wa huduma katika mkakati wa uboreshaji wa huduma hizoPicha: DW/Kizito Makoye Shigela

Hayo yamesemwa kwenye mkutano ulioandaliwa na bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini Tanzania kwa kushirikiana na BoT uliofanyika jijini Arusha kaskazini mwa nchi hiyo na mambo umekamilika hii leo.

Mkutano huo wa kila mwaka unawakutanisha watendaji katika sekta za umma na binafsi zinazohusu masuala ya fedha na uchumi, umefafanua kuwa matumizi ya kidijitali katika utoaji wa huduma za kifedha yatachangia ukuaji wa maendeleo katika sekta hiyo, na kurahisisha utoaji wa taarifa za fedha.

Mada zingine zilizojadiliwa ni pamoja na maendeleo endelevu ya matumizi ya dijitali matika huduma za masoko na hisa ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi, changamoto za matumizi ya kidijitali, uwekezaji endelevu na utoaji wa taarifa, pamoja na matumizi ya teknolojia katika uendelezaji wa makampuni ya fedha katika taifa hilo la Afrika Mashariki.