1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken akaribisha uamuzi wa Ruto kutuliza ghasia Kenya

27 Juni 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amezikaribisha juhudi za Rais William Ruto wa Kenya za kutuliza ghasia zilizosababisha vifo na uharibifu wa mali

https://p.dw.com/p/4hYjm
Katika mazungumzo na Rais Ruto, Blinken amemshukuru Ruto kwa kuchukua hatua za kutuliza mivutano.
Katika mazungumzo na Rais Ruto, Blinken amemshukuru Ruto kwa kuchukua hatua za kutuliza mivutano.Picha: Brendan Smialowski/AP/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amezikaribisha juhudi za Rais William Ruto wa Kenya za kutuliza ghasia zilizosababisha vifo na uharibifu wa mali lakini akahimiza kujiuzuia na kufanyika uchunguzi kuhusu madai ya ukiukaji wa haki. Katika mazungumzo, Blinken amemshukuru Ruto kwa kuchukua hatua za kutuliza mivutano na kuahidi kufanya mazungumzo na waandamanaji na asasi za kiraia.

Ruto amesema Jumatano jioni kuwa anaondoa kabisa mswada wa fedha unaopendekeza nyongeza mpya za kodi ambao ulizusha maandamano makubwa yalisosababisha vifo vya zaidi ya watu 20, na waandamanaji kulivamia bunge. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Mathew Miller amesema Blinken amesisitiza umuhimu wa vikosi vya usalama kujiuzuia na kujiepusha na vurugu. Aidha ametangaza uungwaji mkono wa Marekani wakati Wakenya wakizishughulikia changamoto zao za kiuchumi. Kenya ni mshirika muhimu wa Marekani barani Afrika.