1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blair: Hazitogunduliwa silaha za kuangamiza Iraq:

11 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFk5

LONDON:
Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair anasema huenda ikawa zisigunduliwe tena zile silaha za kuangamiza zinazotafutwa nchini Iraq. Bwana Blair alirudia tena katika Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, kwamba uamuzi wa kuipiga vita Iraq ulikuwa sahihi kutokana na habari za mashirika ya upelelezi kwamba Saddam Hussein hakuteketeza silaha zake zote za kuangamiza, lakini silaha hizo hazikuweko pale ambako jeshi likizitafuta, alisema. Lakini angali anaamini kwamba nchini Iraq zingaliko silaha za kuangamiza, alisisitiza Bwana Blair. Naye Mtawala wa Mambo ya Kiraiya wa Kimarekani nchini Iraq, Paul Bremer amearifu kuwa huenda Saddam Hussein asifunguliwe mashtaka rasmi kabla ya nusu ya pili ya mwaka huu. Kwanza lazima madaraka ya utawala ikabidhiwe serikali ya mpito nchini Iraq, alisema.