1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden kukutana na rais wa Poland mjini Warsaw

21 Februari 2023

Rais wa Marekani Joe Biden anatazamiwa leo kufanya mazungumzo na rais wa Poland Andrzej Duda katika siku ya kwanza ya ziara ya siku mbili nchini Poland.

https://p.dw.com/p/4NmYP
Polen Ankunft Warschau Biden
Picha: Evan Vucc/REUTERS

Baada ya mazungumzo na rais Duda, Biden atatoa hotuba mbele ya kasri la kitamaduni mjini Warsaw inayotarajiwa kuzungumzia pamoja na mambo mengine msimamo wa mataifa ya magharibi kuhusu mzozo wa Ukraine unaolekea kutimiza mwaka mmoja.

Mnamo siku ya Jumatano  rais Biden  amepangiwa kukutana na wawakilishi wa mataifa ya mashariki mwa Ulaya yaliyo wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Biden aliwasili Poland jana usiku baada ya kufanya ziara ambayo haikutangazwa nchini Ukraine, ambako alikutana na rais Volodymyr Zelensky na kumuahidi uungaji mkono usioyumba kutoka Washington.