1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Biden afanya ziara isiyotarajiwa Ukraine

20 Februari 2023

Rais wa Marekani Joe Biden leo amefanya ziara ambayo haijatangazwa nchini Ukraine kama ishara ya kuonesha mshikamano na nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4Nl3M
Ukraine | Krieg | Besuch US Präsident Biden in Kiew
Picha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Kabla ya ziara yake ya Poland ambayo imepangwa, Biden ameizuru Kiev ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini humo tangu Urusi ilipoivamia Ukraine Februari 24.

Rais Joe Biden amekutana na Rais Volodymyr Zelensky na amesema Marekani inasimama na Ukraine na ametangaza msaada zaidi wa kijeshi wenye thamani ya dola milioni 500.

Biden ameihakikishia Ukraine msaada wa Marekani na washirika wake wakati ambapo mzozo huo ukiendelea.

Kwa upande wake Zelensky amesema ziara ya Biden ni ishara muhimu kwa watu wote wa Ukraine. Amesema Urusi haina nafasi ya kuvishinda vita hivyo, baada ya Biden kuahidi msaada zaidi wa silaha.

Aidha, Marekani imesema nchi hiyo iliiarifu Urusi kuhusu ziara ya Biden nchini Ukraine saa kadhaa kabla ya safari hiyo.