1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na China zafikia 'maelewano' kuhusu tabia nchi

10 Novemba 2023

Mjumbe wa Marekani kuhusu masuala ya tabia nchi John Kerry, amesema maelewano hayo yatasaidia kuhakikisha hatua zinapigwa katika mkutano wa COP28 utakaoanza mwisho wa mwezi huu mjini Dubai.

https://p.dw.com/p/4YeiV
Mjumbe wa Marekani kuhusu masuala ya tabia nchi John Kerry
Mjumbe wa Marekani kuhusu masuala ya tabia nchi John KerryPicha: Arnulfo Franco/AP/picture alliance

Kerry alikutana na mwenzake wa China Xie Zhenhua huko Sunnylands, California wiki hii kwa mazungumzo yaliyodumu kwa siku nne, ambayo Kerry alieleza kuwa yalikuwa magumu na mazito.

Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi wamalizika Abu Dhabi

Maelewano kati ya nchi hizo mbili zinazoongoza kiuchumi ulimwenguni, lakini pia zinazotoa  gesi ukaa kwa kiwango kikubwa, yanachukuliwa kuwa muhimu kuelekea mazungumzo ya COP28. 

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kujikita kwenye masuala kama ufadhili wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi na malengo makubwa zaidi ya kuachana na nishati zinazochafua mazingira.