1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden azungumza na Waziri mkuu wa China

11 Septemba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amesema hapo jana kuwa alizungumza na Waziri Mkuu wa China Li Qiang pembezoni mwa Mkutano wa Mataifa 20 yaliyostawi na yanayoinukia kiuchumi G20, huko New Delhi, nchini India.

https://p.dw.com/p/4WB4r
US-Präsident Joe Biden besucht Vietnam
Picha: Luong Thai Linh/AFP

Biden aliwasili mjini Hanoi, nchini Vietnam siku ya Jumapili katika ziara inayolenga kukuza ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili lakini pia kukabiliana na ushawishi wa China katika eneo hilo la Asia Kusini.

Biden amesema Marekani haina nia ya kuihujumu China, lakini akasisitiza kuwa itakuwa vyema pande zote ikiwa Beijing itapata mafanikio kwa kuzingatia sheria za kimataifa.

Uhusiano wa  Marekani na China  umezorota kwa kiasi kikubwa kutokana na masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na China kuiunga mkono Urusi katika vita vyake nchini Ukraine, vitisho vya Beijing dhidi ya Taiwan na migogoro ya kibiashara.