1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden ausifia mkutano wa kilele wa NATO

13 Julai 2023

Rais Joe Biden wa Marekani ameusifu mkutano wa kilele wa nchi za Muungano wa Kijeshi wa NATO kuwa wa kihistoria.

https://p.dw.com/p/4TrbF
Finland USA Präsident Biden in PK
Picha: Antti Aimo-Koivisto/Lehtikuva/AFP

Biden amesema hayo kwenye mkutano na viongozi wa nchi za Skandinavia mjini Helsinki, ambapo ametangaza kuwa viongozi wa NATO wamemkaribisha mwanachama mpya wa muungano huo, Finland, na wamefikia makubaliano ya kusonga mbele juu ya uanachama wa Sweden.

Rais Biden ameeleza kwamba mataifa yanayokutana yanakumbusha siyo tu kwamba yana historia ya pamoja, bali pia yanakabiliwa na changamoto za pamoja na yana maadili ya pamoja.

Soma zaidi: Biden awasili Finland kuhamasisha umoja ndani ya NATO

Rais huyo wa Marekani ameongeza kuwa viongozi wanakwenda sanjari katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Biden anamaliza ziara ya siku tano ya barani Ulaya iliyohusisha kuitembelea Uingereza na kuhudhuria mkutano wa kilele wa mataifa ya NATO katika mji mkuu wa Lithuania, Vilnius.