1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden asema Putin anapoteza vita nchini Ukraine

28 Juni 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amesema Rais Vladmir Putin anashindwa katika vita vyake nchini Ukraine lakini ameongeza kusema ni mapema mno kusema iwapo rais huyo wa Urusi amedhoofishwa na uasi uliotibuka wa kundi la Wagner.

https://p.dw.com/p/4TBW2
Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden.Picha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Alipoulizwa na maripota katika ikulu ya White House iwapo Putin hivi sasa ni dhaifu zaidi, Biden alisema ni vigumu kusema, lakini wazi kwamba anapoteza vita nchini Ukraine na anapoteza pia vita nyumbani.

Biden pia amemtaja Putin kama mtu alietengwa na ulimwengu.

Ikulu ya White inaendelea kuchukuwa tahadhari katika tafsiri yake ya matukio ya wiki iliyopita nchini Urusi, ambako vikosi kutoka kundi la Wagner, mojawapo ya vikosi vyenye uwezo zaidi vya jeshi la Urusi nchini Ukraine, viliasi na kutishia kuishambulia Moscow kabla ya kubadili mwelekeo.

Biden anaongoza kampeni ya mataifa ya magharibi kuiunga mkono Ukraine katika upinzani wake dhidi ya uvamizi wa Urusi ulioanza Februari mwaka uliopita.