1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Biden ampongeza Ramaphosa kuchaguliwa tena Afrika Kusini

15 Juni 2024

Rais wa Marekani Joe Biden amempogeza rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kwa kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili, baada ya chama chake cha AfricaN National Congress, ANC, kuunda serikali ya muungano ya kihistoria.

https://p.dw.com/p/4h5Ef
Marais Ramaphosa na Biden
Rais Ramaphosa alichaguliwa na bunge katika kikao chake cha kwanza kilichofanyika mjini Cape TownPicha: Pete Marovich/UPI Photo/IMAGO

Rais Ramaphosaalichaguliwa na bunge katika kikao chake cha kwanza kilichofanyika Ijumaa mjini Cape Town, kufuatia uchaguzi wa Mei 29, ambamo chama cha ANC kwa mara ya kwanza kilishindwa kupata wingi wa kutosha kuunda serikali kivyake, na kulazimika kutafuta washirika kutoka vyama vya upinzani.

ANC iliungana na chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance - DA, pamoja na vyama vidogo vya Inkatha Freem na vyama vingine vidogo.

Rais Biden amesema katika taarifa kwamba anatazamia kuendeleza ushirikiano kati ya Marekani na Afrika Kusini, kutanua fursa za kiuchumi, kuwekeza katika nishati safi na kuonesha kuwa demokrasia inatimiza.