1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Ramaphosa achaguliwa kwa muhula wa pili Afrika Kusini

15 Juni 2024

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa nchi hiyo kuanza muhula wa pili madarakani.

https://p.dw.com/p/4h48c
Rais Cyril Ramaphosa akiapishwa mbele ya bunge la nchi hiyo baada ya kuchaguliwa kuongoza kwa muhula wa pili
Rais Cyril Ramaphosa akiapishwa mbele ya bunge la nchi hiyo baada ya kuchaguliwa kuongoza kwa muhula wa pili.Picha: Nic Bothma/REUTERS

Uchaguzi huo wa rais unafuatia chama cha Ramaphosa cha African National Congress, ANC, kupata makubaliano na vyama vingine kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Ramaphosa amechaguliwa kwa wingi mkubwa wa kura katika kikao cha kwanza cha bunge jipya la nchi hilo kilichofanyika jana mjini Cape Town, kiasi wiki mbili baada ya kufanyika uchaguzi.

Amepata kura 283 dhidi ya mwanasiasa machachari Julius Malema anayeongoza chama cha mrengo mkali wa kushoto cha Economic Freedom Fighters aliyeambulia kura 44.

Ramaphosa mwenye umri wa miaka 71 amepata ushindi huo kwa kuungwa mkono na chama cha pili kwa ukubwa nchini humo cha Democratic Alliance na vyama vingine vidogo.

Vyama hivyo vilifikia makubaliano ya kuunda seriali ya pamoja na ANC kufuatia chama hicho tawala kukosa wingi wa viti bungeni katika uchaguzi wa Mei 29.