1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden amkabidhi rasmi kijiti Kamala Harris

20 Agosti 2024

Rais Joe Biden ameaga rasmi na kumkabidhi kijiti mgombea urais kupitia chama cha Democratic Kamala Harris katika Kongamano la Kitaifa la Chama hicho huko Chicago siku ya Jumatatu.

https://p.dw.com/p/4jfYx
Biden na Harris
Rais Joe Biden wa Marekani na Makamu wake Kamala Harris, ambaye sasa ndio anayepeperusha bendera ya chama cha Democratic katika kinyang'anyiro cha uraisPicha: Allison Bailey/NurPhoto/IMAGO

Makamu wa rais kamala Harris alijitokeza kwenye mkutano huo na kwenye ujumbe wake mfupi alioutoa mbele ya wajumbe wa chama chake, alimshukuru Rais Joe Biden kwa uongozi wake wa kihistoria na amesema kwa sasa Wamarekani "wanasonga mbele”.

Wasemaji walikuwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Hillary Clinton, aliyempa heshima Harris huku akibainisha uwezo wake wa kuwa rais wa kwanza mwanamke wa Marekani.

Clinton alikuwa mgombea urais wa chama cha Democratic mwaka 2016, lakini alishindwa katika uchaguzi huo na Trump.