1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden, apongeza uamuzi wa ICC wa kutaka kumkamatwa Putin

Angela Mdungu
18 Machi 2023

Raisi wa Marekani Joe Biden, ameupongeza uamuzi wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kwa hatua yake ya kutoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Urusi Vladmir Putin

https://p.dw.com/p/4OsY0
USA Washington D.C. | Präsident Biden beruhigt Weltmärkte wegen Bankenkrise
Picha: Saul Loeb/AFP

Biden amesema, ni wazi kuwa Putin amefanya uhalifu wa kivita na uamuzi wa ICC ni sahihi. Hati ya kukamatwa kwake iliyotolewa jana Machi 17, inazitaka nchi 123 wanachama wa mahakama ya ICC kumkamata rais huyo wa Urusi na kumfikisha  mjini The Hague.

Soma zaidi:ICC yataka Putin akamatwe

Ikulu ya Urusi, Kremlin imesema uamuzi huo ni wa kushtusha lakini hauna maana kwa Urusi.

Nchi hiyo mara kadhaa imekanusha madai kuwa wanajeshi wake wamekuwa wakifanya ukatilikatika uvamizi wake nchini Ukraine ikisema ni operesheni maalumu ya kivita.