1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIreland

Biden akutana na rais na waziri mkuu wa Ireland

13 Aprili 2023

Rais wa Marekani Joe Biden ambaye ana mizizi ya Ireland, leo katika ziara yake ya siku tatu nchini Ireland ameelekea mjini Dublin ambapo amefanya mazungumzo na rais na waziri mkuu wa nchi hiyo kabla kutoa hotuba Bungeni.

https://p.dw.com/p/4Q19Z
US-Präsident Biden besucht Nordirland und Irland
Picha: Brian Lawless/PA Wire/dpa/picture alliance

Baada ya mikutano hiyo Biden akizungumza na waandishi wa habari amelizungumzia suala la kuvujishwa kwa nyaraka za siri za Marekani akisema kwa sasa uchunguzi unaendelea na aliyehusika na uvujishwaji wa nyaraka hizo atatambuliwa karibuni.

Shirika la habari la Reuters limepitia zaidi ya nyaraka 50 ila halijazithibitisha na idadi ya nyaraka zilizovujishwa zinaaminika kuwa zaidi ya 100.

Soma pia:Urusi yatilia mashaka nyaraka za siri za Marekani zilizovuja

Wizara ya sheria ya Marekani ilianzisha uchunguzi baada ya wizara ya ulinzi kuliwasilisha suala hilo kwake na kwa sasa inachunguza hasara iliyotokana na tukio hilo.