1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yatilia mashaka nyaraka za siri za Marekani zilizovuja

12 Aprili 2023

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Ryabkov amesema kiasi kikubwa cha nyaraka za kijasusi za Marekani zilizochapishwa mtandaoni katika wiki za hivi karibuni zinaweza kuwa bandia kwa lengo la kuipotosha Urusi.

https://p.dw.com/p/4PxzZ
Kompyuta na rangi za bendera ya Ukraine
Kuvuja kwa nyaraka za siri za Marekani kuhusu vita vya Ukraine kumeitikisa WashingtonPicha: Jakub Porzycki/NurPhoto/picture alliance

Ryabkov ameyaambia mashirika ya habari ya Urusi kwamba kwa sasa, kuvuja kwa nyaraka hizo kunaibua maswali mengi.

Naibu waziri huyo wa mambo ya nje  wa Urusi amenukuliwa akisema, kwa sababu Marekani inashiriki katika vita vya Ukraine na kwamba inaendesha vita vya propaganda, inawezekana hatua kama hizo zinachukuliwa ili kuipotosha Urusi.

Mapema leo, Ikulu ya Urusi, imesema pia haifahamu kuhusu uhalisi wa nyaraka hizo.

Baadhi ya wataalamu wa usalama wa kitaifa na maafisa wa Marekani wanasema wanashuku huenda raia wa Marekani ndiye aliyehusika katika uvujaji huo lakini pia haondoi uwezekano wa watu wanaoiunga mkono Urusi kuhusika na kitendo hicho.