1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Wahamiaji kupewa msaada wa kujijumuisha

14 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG7f

Wajumbe kutoka sekta za kisiasa,uchumi,biashara na makanisa wamekutana mjini Berlin kwa mkutano mkuu wa kwanza ulio na azma ya kuwajumuisha wahamiaji katika jamii ya Kijerumani.Wajumbe mkutanoni,watajaribu kutafuta njia za kuwasaidia wahamiaji kujifunza vizuri zaidi lugha ya Kijerumani na kuwapatia uwezekano mkubwa zaidi wa kufanya kazi.Mkutano huo wa kilele,uliyozinduliwa na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani umekosolewa kwa sababu baadhi ya jumuiya za kiislamu hazikualikwa.