1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Ujerumani yataka Umoja wa Mataifa kuchukuwa hatua Dafur

26 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFTW

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Yoschka Fischer ameutaka Umoja wa Mataifa kuchukuwa hatua ya kukomesha machafuko ya umwagaji damu kwenye jimbo la Dafur nchini Sudan.

Wito wake unakuja baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kushindwa kukubaliana kutuma wanajeshi wa kulinda amani katika jimbo hilo.Maelfu ya raia wameuwawa na watu wengine wanaokadiriwa kufikia milioni mbili wamepotezewa makaazi yao katika mzozo huo wa miaka miwili.

Hata hivyo Baraza la Usalama limepiga kura kutuma vikosi 10,000 kusini mwa Sudan vikiwa na jukumu la kusimamia makubaliano ya amani yaliotiwa saini kati ya serikali ya Sudan na waasi kusini mwa nchi hiyo makubaliano ambayo yamekomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya zaidi ya miaka 20.