BERLIN: Rais wa Ujerumani ziarani japan.
4 Aprili 2005Rais wa Shirikisho la Jamuhuri ya Ujerumani Horst Köhler amewasili mjini Tokyo kuanza ziara ya siku nne nchini Japan.
Miongoni mwa shughuli zingine rais Köhler atazindua rasmi mradi wa mwaka wa Ujerumani nchini Japan ambao utafuatiwa na mfululizo wa safu 750 za maonyesho kuanzia mwaka ujao zenye lengo la kuboresha mpango wa kubadilishana katika sekta ya utamaduni na elimu baina ya nchi hizi mbili.
Vile vile rais wa shirikisho Horst Köhler atakutana na Mfalme Akihito wa Japan pamoja na waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi.
Kwengineko waziri wa biashara wa Ujerumani Wolfang Clement nae amewasili huko New Delhi kwa ziara ya siku mbili.
Wanao andamana na waziri Wolfang ni kundi la viongozi wa biashara wa Ujerumani. Madhumuni ya ziara hii ni kupanua uhusiano wa kibiashara na kiviwanda baina ya Ujerumani na India.
Waziri Wolfang pamoja na waziri wa fedha wa India Palaniappan Chidambaram wataongoza mkutano wa kibiashara mjini New Delhi. Uhusiano wa kibiashara wa nchi hizi mbili umeongezeka kwa asilimia 22.5 hadi kufikia Euro bilioni 6.2.