1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mpango wa kujumuisha jamii za wahamiaji

14 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG7l

Mkutano wa kwanza wa kilele wenye lengo la kuzijumuisha jamii za kigeni nchini Ujerumani unafanywa katika mji mkuu,Berlin.Leo zaidi ya wajumbe 80 kutoka makundi ya jamii za wahamiaji,makundi ya kidini,viongozi wa kiuchumi na wanasiasa wanahudhuria mkutano huo kuzindua sera zitakazosaidia kujumuisha jamii mbali mbali. Wajumbe mkutanoni watajaribu kutafuta njia za kuwasaidia wahamiaji kujifunza vizuri lugha ya Kijerumani na kuwapa nafasi bora zaidi za kupata kazi.Nchini Ujerumani kuna watu milioni 15 wanaotoka kwenye familia za wahamiaji.Hadi mwaka 2010 inatazamiwa kuwa kila mtu wa pili,chini ya umri wa miaka 40 katika miji mikuu,atatokea familia za aina hiyo.