1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

Benki ya Dunia yaidhinisha dola milioni 700 kwa Mexico

24 Juni 2023

Benki ya Dunia imesema imeidhinisha kuipatia Mexico dola milioni 700 kwa ajili ya mpango wa kukuza sera za umma ili kutengeneza fursa za kiuchumi na kupanua usalama wa kijamii kwa wanawake.

https://p.dw.com/p/4T0hf
Weltbankpräsident David Malpass
Picha: ANDREW KELLY/REUTERS

Mpango huo pia utazingatia kupanua aina ya usafiri unaotoa kiwango cha chini cha gesi chafu.Pia, programu hiyo inatarajiwa kusaidia kuziba mapengo ya kijinsia, kuwezesha upatikanaji wa nafasi bora za ajira, kuboresha usalama kwenye mifumo na usafiri wa umma na kuzuia ukatili wa kijinsia ambao ni suala la dharura katika taifa hilo. Nchini humo, inaripotiwa kuwa wastani wa wanawake 20 huuwawa kila siku.

Soma zaidi:Benki ya Dunia na IMF yahangaikia uchumi wa dunia

Mpango unaangalia pia kupanua usalama wa kijamii kwa manufaa ya wafanyakazi wote wa nyumbani ambao wengi wao ni wanawake na kuwalinda dhidi ya hali ngumu ya kiuchumi.  Kulingana na idara ya takwimu nchini humo, asilimia 72 ya wafanyakazi wa nyumbani hawana aina yoyote ya mafao ya kazi.