1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

NATO yakemea matamshi ya Urusi kuhusu Nyuklia

27 Machi 2023

Jumuiya ya Kujihami ya NATO imekemea kauli za Rais wa Urusi Vladimir Putin baada ya kiongozi huyo kusema atapeleka nchini Belarus silaha za kimkakati za nyuklia.

https://p.dw.com/p/4PJnK
Norwegen | Jens Stoltenberg und Ursula von der Leyen besuchen norwegische Gas-Plattform
Picha: Ole Berg-Rusten/NTB Scanpix/AP/picture alliance

Kutokana na kauli hiyo, Ukraine imetoa wito wa kufanyika Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ameionya Belarus kwamba inaweza kukabiliwa na vikwazo zaidi iwapo itakubali kuzipokea silaha hizo.

Hayo yanajiri wakati mapigano yakiendelea nchini Ukraine. Leo Jumatatu, watu wawili wameuawa na wengine 29 wamejeruhiwa baada ya Urusi kuushambulia kwa makombora mji wa Sloviansk, kaskazini magharibi mwa Bakhmut.