1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut:Umoja wa nchi za kiarabu kukutana na UN.

8 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDNa

Ujumbe wa umoja wa nchi za kiarabu unatazamiwa kuwasili Umoja wa Mataifa hii leo kutoa mapendekezo yao yatakayopelekea kumalizika kwa mgogoro wa mashariki ya kati.

Lebanon umeyaita mapendekezo hayo kuwa ni ya upande moja kati ya Marekani na Ufaransa, hususan kwa vile mapendekezo hayo hayaitaki Israel kusimamisha mashambulizi yake na kuondoka haraka nchini Lebanon.

Jana serikali ya Beirut ilisema inajitayarisha kupeleka wanajeshi wake 15,000 ili kuunga mkono vikosi vya Umoja wa Mataifa huko kusini mwa Lebanon wakati vikosi vya Israel vikiondoka.

Hata hivyo Israel imekataa kuondoka maeneo ya kusini mwa Lebanon hadi pale jeshi la kimataifa litakapokaa na maeneo hayo na kuilinda Israel na mashambulizi ya Hezbollah.