1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Baraza la Usalama laomba ushauri wa kukabiliana na Taliban

17 Machi 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limemuomba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kutoa tathmini huru ya namna ya kuushughulikia utawala wa Taliban nchini Afghanistan.

https://p.dw.com/p/4Ope0
Afghanistan Kabul | Taliban Kämpfer in der Stadt
Picha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa aidha limeomba kushauriwa namna linavyoweza kupambana na changamoto ikiwemo ukandamizaji wake wa haki za wanawake na wasichana. Baraza hilo lenye nchi 15 wanachama lilipitisha kwa kauli moja azimio linalomhitaji Guterres kuwasilisha ripoti katikati ya mwezi Novemba, ikiwa na mapendekezo ya mbinu za kufanya kazi na utawala huo katika nyanja muhimu kama siasa, kibinaadamu na maendeleo ndani na nje ya Umoja wa Mataifa. Utawala wa Taliban uliochukua madaraka Agosti mwaka 2021 wakati wanajeshi walioongozwa na Marekani kuondoka nchini humo baada ya miaka 20 ya vita, unasema unaheshimu haki za wanawake chini ya tafsiri yake ya sheria za kiislamu.